Hospitali Ya Rufaa Ya Mkoa,Bukoba BRRH
Huu ni ukurasa rasmi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba. Karibu kwa huduma bora
02/08/2026
HABARI PICHA: Menejimenti Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Bukoba, ikiwa katika kikao cha tathmini ya Kimatibabu (Clinical Audit) kilichoendeshwa na watumishi kutoka Wizara ya Afya ikikiwa na lengo la kupima, kutathmini na kuboresha ubora wa huduma za afya zinazotolewa kwa wananchi.
28/07/2026
SIKU YA HOMA YA INI DUNIANI.Wizara ya Afya Tanzania
27/07/2026
TANGAZO LA KAZI KWA VIJANA WA KUJITOLEA
25/07/2026
WATUMISHI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA WAPEWA ELIMU KUHUSU NJAA ILIYOJIFICHA
Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba wamepatiwa elimu kuhusu njaa iliyojificha (Hidden Hunger) kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu umuhimu wa ulaji wa lishe bora na madhara ya upungufu wa vitamini na madini muhimu mwilini.
Elimu hiyo imetolewa na Maafisa Lishe wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba wakati wa kikao cha elimu endelevu kwa watumishi (Continuing Medical Education - CME) kinachofanyika kila siku ya Ijumaa hospitalini hapo.
Akitoa elimu hiyo, Afisa Lishe wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Victoria Ngatunga amesema njaa iliyojificha ni hali ambayo mtu anakula chakula cha kutosha na kushiba, lakini mwili wake unakosa vitamini na madini muhimu k**a vile madini chuma (Iron), vitamini A, foliki asidi (Folic Acid) madini joto (iodine) na zinki yanayohitajika kwa ukuaji, kinga ya mwili na utendaji mzuri wa viungo mbalimbali.
Ameeleza kuwa hali hiyo mara nyingi haitambuliki kirahisi kwa sababu mtu anaweza kuonekana mwenye afya njema, lakini akawa na upungufu wa virutubisho muhimu unaoweza kusababisha uchovu wa mara kwa mara, upungufu wa damu, kinga dhaifu ya mwili, matatizo ya ukuaji kwa watoto, kupungua kwa uwezo wa kufikiri na kufanya kazi pamoja na kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mbalimbali.
Victoria amesema mtu anaweza kushukiwa kuwa na njaa iliyojificha iwapo hupata uchovu usioelezeka, kuugua mara kwa mara, ana upungufu wa damu, ngozi na nywele kuwa dhaifu, kuchelewa kupona majeraha au baada ya kufanyiwa vipimo kubainika kuwa ana upungufu wa vitamini au madini muhimu mwilini.
Kwa upande wake Unice Philbert ambaye pia ni Afisa Lishe hospitali ya Mkoa, Bukoba amesisitiza kuwa njia bora ya kujikinga na njaa iliyojificha ni kula mlo kamili unaojumuisha makundi yote ya vyakula, hususan matunda na mboga za majani, vyakula vya asili ya wanyama na mimea vyenye madini na vitamini mbalimbali, kutumia chumvi ambayo imeongezewa madini joto.
USIKOSE KUFUATILIA KIPINDI CHA CHUMBA CHA DAKTARI KESHO SIKU YA JUMANNE TAREHE 14.07.2026 SAA 10:15 JIONI HADI SAA 11:00 JIONI NDANI YA REDIO MBIU ATAKUWEPO DAKTARI BINGWA WA MACHO DANIEL MASHAMBA AKITOA ELIMU YA MAGONJWA YA MACHO NA JINSI KUEPUKANA NA MAGONJWA YA MACHO
10/07/2026
*MENEJIMENTI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA, BUKOBA YATAMBUA MCHANGO WA IDARA, VITENGO NA WATUMISHI WANAOFANYA VIZURI KATIKA UBORESHAJI WA HUDUMA*
Menejimenti ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba imetambua na kuzipongeza idara, vitengo pamoja na watumishi waliofanya vizuri katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wateja kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
Hafla hiyo iliyoandaliwa na Kitengo cha Usimamizi wa Ubora wa Huduma (Quality Improvement Unit - QIU), imelenga kutambua na kuthamini mchango wa idara, vitengo na watumishi waliodhihirisha weledi, uwajibikaji na kujituma katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora na stahiki.
Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Usimamizi wa Ubora wa Huduma (QIU), Bi. Vivina Rwehumbiza, amesema kuwa baada ya tathmini iliyofanyika, vitengo vitatu vilivyofanya vizuri zaidi kwa mwaka wa fedha 2025/2026 ni Idara ya Maabara, Idara ya Huduma za Dharura (Emergency Department) na Private Ward.
Bi. Rwehumbiza amesema utambuzi huo ni sehemu ya kuhamasisha utamaduni wa kufanya kazi kwa ubora na kuendelea kuboresha huduma zinazotolewa hospitalini, huku akiwataka watumishi wote kuendelea kushirikiana ili kufikia viwango vya juu zaidi vya utoaji huduma.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba, Dkt. Museleta Nyakiroto, amezipongeza idara, vitengo na watumishi wote waliotambuliwa kwa kujituma na kutekeleza majukumu yao kwa weledi na ufanisi.
Dkt. Nyakiroto amesema mafanikio hayo yanapaswa kuwa chachu kwa idara na vitengo vingine kuongeza bidii na kujifunza kutoka kwa wenzao waliopata tuzo, ili hospitali iendelee kutoa huduma zenye ubora, usalama na zinazokidhi matarajio ya wananchi.
Amesisitiza kuwa Menejimenti itaendelea kuweka mazingira yanayochochea utendaji bora na kutambua mchango wa watumishi wanaofanya kazi kwa bidii, hatua ambayo itasaidia kuimarisha utoaji wa huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba.
02/07/2026
KARIBU KARIBU KWENYE BANDA LETU TUKUHUDUMIE
26/06/2026
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba inakupongeza Dkt. Grace Magembe kwa Kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Afya.
25/06/2026
SIKU YA VITILIGO DUNIANI
19/06/2026
WATUMISHI BRRH WAPATIWA ELIMU YA NAMNA YA KUMBAINI MHUSIWA WA UGONJWA WA EBOLA
Wataalamu wa afya 57 kutoka Hospitali ya Rufaa ya ya Mkoa, Bukoba wamepatiwa elimu kuhusu namna ya kuweza kumbaini na kumtambua mhisiwa wa ugonjwa wa Ebola huku wakisisitiza kuwa , muhisiwa hutambuliwa kwa kuzingatia dalili maalum za kiafya sambamba na historia ya mtu huyo, hususan k**a ametokea au ametembelea eneo ambalo mlipuko wa ugonjwa wa Ebola umethibitishwa kuwepo.
Akitoa elimu juu ya kumtambua muhisiwa Dkt. Philipo Lambo Shineneko ambaye pia ni mtaalam wa Epidemiolojia kutoka Wizara ya Afya amesema kuwa, mhisiwa wa Ebola anaweza kuonyesha dalili zifuatazo: homa kali ya ghafla ya nyuzi joto 38 pamoja dalili mbili kati ya zifuatazo, maumivu makali ya kichwa, uchovu usio wa kawaida, maumivu ya misuli na viungo, kutapika, kuharisha, maumivu ya tumbo pamoja na kutokwa na damu kwenye fizi, pua, macho au sehemu nyingine za mwili katika hatua za baadaye za ugonjwa.
Imeelezwa kuwa si kila mtu mwenye dalili hizo huhesabika moja kwa moja kuwa ana Ebola, bali mtu huchukuliwa kuwa mhisiwa pale anapokuwa na dalili hizo na wakati huo huo amekuwa katika eneo lenye mlipuko wa Ebola, au kutangamana na mgonjwa wa Ebola au mtu aliyefariki kwa ugonjwa huo.
Wataalamu hao pia wamefundisha hatua muhimu za kuzingatia endapo mhudumu wa afya au mwananchi atakutana na mhisiwa wa ugonjwa wa Ebola. Hatua hizo ni pamoja na kuchukua tahadhari kinga kabla ya kugusa mwili wa mhisiwa kwa kuvaa vifaa kinga, kumtenga mara moja mhisiwa na watu wengine, kutoa taarifa kwa mamlaka husika za afya kwa haraka, kuchukua taarifa za mhisiwa na za waliotangamana naye katika fomu maalum zilizosambazwa vituo vya kutolea huduma, pamoja na kuhakikisha mhisiwa anapelekwa kwenye kituo cha afya kilichoandaliwa kushughulikia magonjwa ya mlipuko.
Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa, Bukoba Dkt. Museleta Nyakiroto amemshukuru Dkt. Philipo Lambo Shineneko pamoja na Wizara ya Afya kwa kuendelea kutuma
Click here to claim your Sponsored Listing.
Website
Address
Bukoba